Share this on:
 E-mail
57
VIEWS
 
RECOMMENDS
2
SHARES
About this iReport
  • Not vetted for CNN

  • Click to view MashuaFgm's profile
    Posted February 6, 2010 by
    Location
    Dallas, Texas
    Assignment
    Assignment
    This iReport is part of an assignment:
    Your photos from 'Inside Africa'

    More from MashuaFgm

    Maadhimisho ya kukomesha UKEKETAJI duniani Feb 6, FEMALE GENITA MUTILATION (SWAHILI version)

     

    UKEKETAJI.....hauna faida mbali maafa kibao katika Afya ya wanawake , Ungana nami kukomesha ukeketaji..elimisha jamii madhara ya kiafya na vifo vinavyotokana na UKEKETAJI!
    http://twitter.com/Mashua
    http://www.facebook.com/pages/Mashua-...
    Ukeketaji unakwenda kinyume cha uumbaji wa Mungu. Mungu akamuumba mtu kwa
    mfano wake.
    Ukeketaji unakiuka haki za mwanamke na msichana kama zinavyoelezwa katika mkataba
    wa kimataifa dhidi ya ubaguzi wa aina zote kwa wanawake wa mwaka 1979 (CEDAW)
    Mkataba wa kimataifa juu ya haki za mtoto wa 1989 na tamko la kiafrika juu ya haki na
    ustawi wa mtoto. Ukeketaji unasababisha maumivu ya kudumu ulemavu na hata vifo.
    Kipekee ukatili huu unavunja haki, utu na heshima ya mwanamke na mtoto.
    c. Ukeketaji una madhara mengi kwa wanawake na wasichana na watoto wanaotendewa
    jambo hilo. Wanawake waliokeketwa wanaathirika kiafya, kisaikolojia, kijamii na
    kiuchumi na mengineyo kwa mfano:
    - Athari za kiafya ni pamoja na:
    i. Maumivu makali wakati wa kukeketwa
    ii. Kuvuja damu nyingi wakati wa kukeketwa na wakati wa kujifungua
    iii. Kupata makovu ambayo huchanika vibaya wakati wa kujifungua Kuvimba maeneo ya
    siri kama tunavyoona wengine wanaovimba masikio wakati wanapotoga masikio yao.
    iv. Kupata maambukizi ya magonjwa hasa VVU wakati wa kukeketwa na mengineyo.
    Athari za kijamii baadhi ni kama zifuatazo:
    i. Tendo la ndoa kukosa msisimuko au raha kwa mwanamke na kuwa kero
    ii. Kukosa watoto ukeketaji unapokosewa.
    Athari za kisaikolojia ni pamoja na:
    i. Mwanamke kuwa na maumivu ya kudumu
    ii. Kuchukia tendo la ndoa
    iii. Kujisikia kutotoshelezwa wakati wa tendo la ndoa.
    Madhara au athari hizi zinakuwa jinamizi linalomfuata mwanamke maisha yake yote.
    Balozi Lucy Mashua ,
    Balozi wa kukabiliana na ukeketaji duniani.
    Msaidizi wa wakimbizi hapa Marekani
    Mwenye kiti wa kamati inoyopinga ukeketaji duniani.

    What do you think of this story?

    Select one of the options below. Your feedback will help tell CNN producers what to do with this iReport. If you'd like, you can explain your choice in the comments below.
    Be and editor! Choose an option below:
      Awesome! Put this on TV! Almost! Needs work. This submission violates iReport's community guidelines.

    Comments

    Log in to comment

    iReport welcomes a lively discussion, so comments on iReports are not pre-screened before they post. See the iReport community guidelines for details about content that is not welcome on iReport.

    Add your Story Add your Story